Uongozi wa Yanga utakutana na kujadili na mwisho
kupata jibu ni aina gani ya uwanja inataka kati ya ramani nne ilizopewa na wajenzi
wa Kichina.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zimeeleza,
suala hilo limekuwa ni siri kubwa na baada ya siku saba, jibu litarudishwa kwa
Wachina hao hao.
“Tutakutana na kujadili kuhusiana na suala hilo,
unajua Yanga ina wataalamu wengi ambao wangependa kuamua mambo yao kwa
ushirikiano na kukubaliana.
“Kila mtu atakuwa na nafasi ya kutoa maoni yake kwa
kuwa pamoja na ramani zile tatu, lazima suala la gharama litaangaliwa na
tutachagua.
“Mwisho tutawasiliana na hao Wachina na kuwaambia
tumechagua ramani ipi na nini kinafuatia baada ya hapo,” kilisema chanzo.
Siku chache zilizopita, Kampuni ya Wachina ya
Beijing Construction Engineering Group (BCEG) iliwapa Yanga ramani ya viwanja
vitatu, cha gharama zaidi kikiwa kinagharibu dola 50,000 (zaidi ya Sh bilioni
81) ili wachague wanachokihitaji.
Ramani
nyingine thamani yake ilikuwa ni milioni 40,000 yenye uwezo wa kuchukua watu
40,000 na ya mwisho ni thamani yake ni dola milioni 30,000 yenye uwezo wa kuchukua
watu 30,000.
0 COMMENTS:
Post a Comment