April 7, 2013




Kocha wa Real Madrid, José Mourinho amechagua wachezaji 21 atakaosafiri nao hadi Istambul, Uturuki kuwavaa Galatasaray katika mechi ya pili ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kati ya hao, Mourinho amewashangaza wengi kwa kuamua kuchukua makipa wanne, lakini amemuacha kiungo wake Mbrazil, Ricardo Kaka ambaye ni majeruhi.


Madrid ilishinda kwa mabao 3-0 katika mechi ya kwanza iliyopigwa mjini Madrid, Hispania.
Katika mazoezi ya juzi asubuhi, wachezaji Mesut Özil, Pepe, Kaká na Ricardo Carvalho walijifua tofauti na wenzao kutokana na kutokuwa fiti katika kiwango cha kutosha.

Lakini wachezaji hao watatu, wote walicheza katika mechi ya La Liga ambayo Madrid iliibuka na ushindi wa mabao 5-1.

Mchezaji mwingine ambaye hatasafiri na Madrid kwenda Istambul ni Sergio Ramos ambaye ana kadi za njano zinazomzuia kucheza mechi hiyo ya marudiano.

Kikosi kamili alichokichagua Mourinho kwa ajili ya mechi hiyo ya Istambul:
The Real Madrid squad named for the Galatasaray game is:

Casillas, Diego López, Adán and Jesús (MAKIPA).
Varane, Pepe, Coentrão, Marcelo, Arbeloa, Albiol and Nacho (MABEKI).
Khedira, Özil, Essien, Modric, Callejón and Di María (VIUNGO).
Cristiano Ronaldo, Benzema, Higuaín and Morata (WASHAMBULIAJI).

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic