May 5, 2013



Timu ya Azam FC inatarajiwa kutua nchini kesho (Mei 6, mwaka huu) saa 7 mchana kwa ndege ya Emirates kutoka Morocco ikipitia Dubai ambako ilibadili ndege.

Azam FC ilikuwa nchini Morocco kucheza mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya AS FAR Rabat ya huko na kulala kwa mabao 2-1.

Kutokana na kupoteza mchezo huo, Azam FC imeondolewa katika michuano hiyo kwa kuwa katika mechi ya awali dhidi ya Waarabu hao wa Morocco matokeo yalikuwa suluhu.

Hata hivyo, Azam FC watalazimika kujilaumu wenyewe kwa kuwa walifanikiwa kupata penalti lakini ikapotezwa na John Bocco.

Kama wangefanikiwa kutoa sare ya aina yoyote ya mabao, Azam FC wangefuzu na kuendelea kuwa wawakilishi pekee wa Tanzania na Afrika Mashariki katika michuano ya kimataifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic