May 5, 2013



Samatta akiwa mpira na kipa wa Orlando..
 Pamoja na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Orlando Pirates ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumba, TP Mazembe imetolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
 
KImwaki Mpela akimthibiti Collins Mbesuma..
Mazembe anayochezea Mtanzania, Mbwana Ally Samatta imetolewa kwa kuwa ilitakiwa kushinda mabao 2-0 ili kusonga mbele baada ya kuwa imepoteza kwa mabao 3-1 katika mechi ya kwanza jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

Mazembe walipoteza mkwaju wa penalty, bado nahodha wa Orlando Pirates, Lucky Lekgwath akalambwa kadi nyekundu katika dakika ya 28.
 
KImwaki Mpela wa Mazembe na Rudolf Bester
Mazembe walifunga bao lao katika dakika ya 73 kupitia kwa Kasusula lakini wenyeji hao walipoteza mikwaju miwili ya penati yote ikipanguliwa na kipa wa Pirates, Senzo Meyiwa.


Mkwaju wa kwanza wa penalti uliotolewa na mwamuzi kutoka Shelisheli ulipigwa na Eric Bokanga kipa huyo akaokoa, mkwaju wa pili akapiga nyota wa Mazembe, Tresor Mputu nao ukapanguliwa na kipa huyo.

Pamoja na hivyo Mazembe bado walishindwa kuzitumia nafasi walizozipata kupata bao hilo ambalo lingewavusha.

Mitandao ya Afrika Kusini iliripoti kwamba kuna mwandishi mmoja amekamatwa na kukataliwa kurekodi mechi hiyo na alikuwa anashikilia hadi baada ya mchezo huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic