Saa
24 tu baada ya kutwaa ubingwa wa Europa League, wachezaji wa Chelsea akiwemo Frank
Lampard, Juan Mata na Oscar wamezawadiwa tuzo nyingine.
Hafla
ya tuzo hizo ilifanyika jana usiku na wachezaji hao wakazawadiwa kutokana na
kazi yao katika klabu hiyo ambayo imetwaa makombe mawili makubwa barani Ulaya
katika miaka miwili.
Katika
sherehe ya tuzo hizo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, Mata alilamba
tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Chelsea ikiwa ni kwa mara ya pili mfululizo.
Kiungo
Mbrazil, Oscar alishinda tuzo ya vao bora la msimu na kinda, Nathan Ake aliteuliwa
kuwa mchezaji bora wa mwaka anayechipukia.
Frank
Lampard naye alikabidhiwa tuzo ya heshima ya kuweka rekodi ya kufunga mabao
mengi na kuvunja rekodi ya Bobby Tambling.
Chelsea
ilifanikiwa kushinda mabao 2-1 dhidi ya Benfica mjini Amsterdam na kubeba kombe
hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment