Mwamuzi Martin Saanya atakayechezesha pambano la watani Simba na
mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga, Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam ni askari magereza.
Salehjembe limebaini kazi ya Saanya ambaye ni askari wa jeshi hilo
mkoani Morogoro na aliyebadilishwa Israel Mujuni Nkongo ni mwalimu.
Saanya ndiyo mwamuzi wa mchezo huo na tayari Simba imeandika barua TFF
kupinga mwamuzi huyo kuingizwa katika nafasi ya Nkongo, tena ghafla.
Mwamuzi huyo ilikuwa kazi kumpata, kila alipopigiwa simu hakupokea
lakini kachero wa Salehjembe alifanikiwa kumnasa mjini Morogoro, naye
akazungumzia mchezo huo kwa kifupi tu.
“Najua ni mchezo ambao unatazwa na watu wengi sana, nitakachofanya ni
kufuata haki tu na si vingine,” alisema Saanya akikataa kuzungumza zaidi.
Baadhi ya rafiki zake wa karibu hasa wale waamuzi pia, walimtambulisha
Saanya kama mwamuzi anayefuata sheria sana, asiyekubali kuyumbishwa.
Hivyo wachezaji wa Yanga na Simba wanapaswa kuwa makini kwani anaweza
asisite kumwaka kadi kama njugu kama wachezaji hao hawatacheza soka na kuleta ‘mambo
mengine’.
0 COMMENTS:
Post a Comment