May 12, 2013






Sare ya Real Madrid ya mabao 1-1 dhidi ya Espanyol imewapa nafasi Barcelona kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa La Liga.

Barcelona wamekuwa mabingwa wakati nyumbani ‘wanakunywa chai’, kwani sare hiyo imeifanya Madrid ifikishe pointi 81 ikiwa imecheza mechi mbili mbele zaidi na Barca yenye pointi 88.


Hivyo hata kama Madrid itashinda mechi zake zilizobakia haitaweza kufikia ilizonazo Barca.

Hilo ni taji la 22, maana yake Barcelona imeweka rekodi mpya katika karne kwa kuwa timu iliyotwaa mara nyingi zaidi ubingwa wa La Liga.


Wakati wa mchezo huo, Mourinho alimuweka nje mshambuliaji wake nyota, Cristiano Ronaldo, lakini baada ya kuona wameshafungwa alimuingiza ili kuokoa jahazi lakini mwisho ikawa ni sare hiyo baada ya Higuain kusawazisha.

Baada ya mchezo huo, mashabiki wa Barcelona waliingia mitaani na kuanza kushangilia ubingwa huo ambao wameipokonya Real Madrid.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic