Bayern Munich wameonyesha bahati mbaya si kila siku
baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Borussia Dortmund katika
fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Wemblery jijini
London, mabao yote yalifungwa katika kipindi cha pili, Bayern wakianza katika
dakika ya 60 kupitia Mandzukic na BVB wakasawazisha dakika nane baadaye kupitia
Grosskreutz kwa mkwaju wa penalty.
Mholanzi Aarjen Robben ndiye alimaliza kazi katika
dakika ya 89 baada ya kufunga bao maridadi.
Bayern ambayo imekuwa na bahati mbaya, kwani hata
msimu uliopita ilikosa kombe hilo katika hatua za mwisho baada ya kufungwa na
Chelsea.
0 COMMENTS:
Post a Comment