November 12, 2020


ANAANDIKA Saleh Jembe

 KATIKA hili suala la Senzo (Mbatha) na Mbaga (Hashim) kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za upangaji matokeo (match fixing) ni vizuri sana TUKAHESHIMU jeshi lenyewe na wahusika wenyewe.


Kwanza:
Senzo na Mbaga ni watuhumiwa, bado hawajahukumiwa na tuendelee kuwa na subira badala ya kuingiza ushabiki wa Uyanga na Usimba.

Naona wengine wanawatetea na wengine wanawakandamiza. Vizuri tulipe nafasi jeshi hilo kupitia wataalamu wake ili tupate majibu sahihi.

Pili:

Tuache propaganda katika hili, kwamba Senzo anataka kufukuzwa, na kadhalika. Anayesema anahusishaje na tuhuma za upangaji matokeo. Msizushe maneno kwa jeshi lenyewe au watuhumiwa.

Tatu:
Tupunguze kusema maneno yasiyo na ukweli ili mradi tunaweza kuandika. Jeshi la Polisi litatoa majibu na mwisho tutapata uhakika na si kila mmoja kusema analojua.

Match fixing ni adui wa mpira wetu na duniani kote. Kama polisi wanafanya uchunguzi tuwape muda ili mwisho uwe sahihi na usio na shinikizo kwa maana ya kuwa tunataka majibu ya haki nini haki ili tujue ukweli WALIHUSIKA kweli au zilikuwa HISIA tu.

13 COMMENTS:

  1. Hivi kuna timu duniani isiyofungwa? Sasa hawa jamaa wakifungwa wanatafuta mchawi. Labda wakaishi mwezini.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeelewa kilichoandikwa hizo ni tuhuma sasa wewe ushakuja na hitimisho lako

      Delete
    2. Wamechanganyikiwa! Badooo, watapigwa sana tu, kwanza washavurugana.

      Delete
  2. Juha mkubwa wewe usichoelewa hapo ni nini au unaandika tu ilimradi kujifurahisha ama?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe ndio kilaza... ile penalt aliyokosa bocco nayo walimtetemesha miguu

      Delete
  3. Juu ya Simba kucheza chini ya kiwango, lakini si tulishuhudia jinsi Gongowazi walivoelemewa na kupatiwa peneti ya aibu na baadae Mnyama alipobadilisha kasi ya kuelemea na kupata bao la uhakika na juu ya hayo wale jamaa wanajinasibu wameifunga Simba.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tukumbushe na matukio yaliyotokea kwenye ile mechi iliyoisha kwa sare ya 2-2

      Delete
    2. Acha ukiazi ww refa ndani ya dk 90 alilipa.

      Delete
    3. Simb awanachekesha sana, ile penalti ya Kagere msimu ule ilitakaswa , hii ndio imekuwa gumzo hadi mnata VAR, hahahahaa kuli akupokezana, jiandaeni kisaikolojia!

      Delete
  4. penalti ya Kisinda imetokea nje kabia kama mita moja na zaidi nje ya mstari wa 18..Penalti ya Kagere ilikuwa nje lakini katika 18...video bado ziko youtube kaangalie..Pia katika mechi hiyo mwamuzi hakuwanyima Yanga penalti...Hii mechi mbali na kuwanyima Simba penalti mwamuzi pia alikuwa anawaharibia Simba mashambulizi pale zinapotokea faulu bubu..kama nne Simba wakuanza anazuia,Sasa kama siyo hujuma na alikuwa amehongwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wafanyaji hujuma wamkifanyiwa hujuma wanamaindi balaa, wanaumia sana, miaka yote mitatu mmeshinda kwa hujuma, ni kama tu mwizi akiiba hataki kuibiwa, hahahahaha! raha sana! Miaka mitatu mfululizo boss wenu MO katumia hela sana mkafanya figisu zote , hapo Yanga walikuwa hawana hela. Sasa wamepatikana watu wenye hela na wanajua figisu, mnakimbilia police na kuanza kulalama. Msimu uliopita Simba walihakikisha Yanga wanapoteza michezo mingi na kupata droo za kumwaga kwa kila namna. Bora tu mutulie dawa iwaingie, kudadadadeki!

      Delete
    2. Tino una ushahidi refa kahongwa? Tulieni dawa ipenye kudadadadeki!

      Delete
  5. Kwanza hadi sass matokeo ya Zlatico na mazuri zaidi ukilinganisha na jumla ya michezo aliyofundisha na ile ambayo amishacheza Kaze.Tusijidanganye mwaka juzi zikiwa bado mechi nne ligi kuisha Yanga walikuwa wanajua wanamatumaini ya kuchukua ubingwa...sare zilishaanza na kocha huyo mtamtimua tu...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic