May 6, 2019


FT Lipuli 2-0 Yanga
Uwanja : Samora
Kipindi cha pili Zinaongezwa dakika 6

Dakika ya 80 Zawadi ametolewa anaingia Steve wa Lipuli Dakika ya 80 anatoka Miraji Athuman anaingia Nolfant Lufunga. Haji Mwinyi anakwenda benchi anaingia Kelvin Yondan dakika ya 70.

Abdalah Haji anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea rafu Paul Nonga wa Lipuli dk ya 66.

Jimmy Mwaisondola wa Lipuli anaonyeshwa kadi ya njano dk ya 56 kwa kumchezea rafu Feisal Salum

Amiss Tambwe anaingia akichukua nafasi ya Mohamed Banka

Zimeongezwa dakika 4

Miraj Athuman Goooaaaal dk ya 39

Paul Nonga Gooaaal dk ya 29

MCHEZO kwa sasa Uwanja wa Samora ni kipindi cha pili, mkoani Iringa ni kati ya Lipuli na Yanga hatua ya nusu fainali kombe la Shirikisho.

Paul Nonga anawanyanyua mashabiki wa Lipuli dakika ya 29 baada ya piga nikupige kwenye lango la Yanga.

Miraj Athuman anaandika bao la pili kwa Lipuli baada ya mabeki wa Yanga kufanya makosa kama ya awali kuzembea kuokoa mpira.

Mashabiki wamejitokeza kwa wingi kuona namna nusu fainali ya kibabe inavyopigwa kwa wababe hawa wawili.

24 COMMENTS:

  1. Dakika 15 Za Zahera Zamumaliza Mwenyewe Wataendelea Kushabikia Timu Ngeni

    ReplyDelete
  2. Yanga anacheza na timu tatu hapa lipuli,simba na TFF

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha umama wewe..

      Delete
    2. Hamna mchezaji wa Simba au benchi la ufundi wa Simba pale.Tena Yanga wamebebwa!Free kick na tuongelee dakika zilizoongezwa!Au inapendelewa Simba zikiongezwa nyingi!

      Delete
    3. Hata acheze na timu kumi kafungwa acha kutafuta sababu.Hio ndio kukaribisha uongozi mpya

      Delete
    4. Yanga mtasema mengi ila hata kama Simba kaisaidia lipuli ili iwaadhibu basi ni haki yao kwani mlizidi sana vitimbwi kwenye klabu bingwa Africa. Yaani mtenda akitendewa hujihisi kaonewa na kusahau aliyokuwa akiyafanya.Ila kilichowafanya Yanga kupoteza mechi na lipuli ni pressure au msongo wa mawazo kwa wachezaji wa Yanga hasa juu mustakabali mzima juu ya mwenendo wa ligi kuu na jinsi Simba inavyokwenda kuwaondosha kwenye usukani wa ligi kuelekea ubingwa. Yanga tangu awali hakuwa na timu iliyoundwa kwa ajili ya mapambano ya muda mrefu kwa mashindano tofauti ni kama dhali tu yanga kuongoza ligi mpaka hivi sasa na tulijua furaha ya wanayanga itageuka mauzi endapo tu Simba atarudi kikamilifu kwenye ligi na ndicho kilichotokea. Kwa hivyo poleni sana wanayanga ila mmeyataka na hicho kiherehere chenu cha kutaka kula sahani moja na Simba kwani uwezo huo kwa sasa hamna mtaumia bure.

      Delete
  3. Timu hizi Kila mmoja anamuombea njaa mwenzake, wewe fanya kazi yako. Kama umemuona refa was mbeya city alivyokuwa mkali kwa magoli halali inaonyesha waliahidiana kitu na yanga Sasa kikaingia mdudu baada ya kupigwa ndo maana alichukia sana

    ReplyDelete
  4. Uwanjani Sijaona Mchezaji Yeyote Wa Simba Wala Kiongozi Yeyote Wa Tff Wachezaji Wapo 11 Wa Lipuli Na Wa Yanga 11 Kindoki Man Of Match Wa Uzembe Leo Tunawatakia Kheri Mashabik Wayanga Ktk Kusapoti Wageni Simba Inapocheza Kimatafa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndio sasa mwakani watapanda ndege kwa fadhila ya Simba !

      Delete
  5. Eti Zuhura alisema watamaliza mechi baada ya dak 15

    ReplyDelete
  6. TFF,Simba oyeee maombi yenu yametimia leo

    ReplyDelete
  7. Idara mpya ya yanga imekaribishwa Kwa shubiri badala ya haluwa

    ReplyDelete
  8. Wameongezwa dak 6 mpira umcheza hadi ya 7! Hawajaonewa kabisa..Na walipewa free kick ambayo angepiga Ajib!

    ReplyDelete
  9. Ndiyo sasa watapanda ndege michuano ya kimataifa kwa fadhila ya Simba...Ile waliyokuwa wanaenda kwa Mkapa kuwashangilia Nkana ,AS Vita na Al Ahly utadhani wageni hao walikuja na meli iliyojaa mashabiki Dar

    ReplyDelete
  10. Na hiyo fadhila sio kwa msimu huu wa 2019 / 2020, ni hadi msimu wa 2020 / 2021. na hapo wafanye vizuri kwenye ligi wawe nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi ya Tanzania kwa msimu wa 2019/2020.

    Wanaposema kuwa wamecheza na timu tatu (TFF, Simba na Lipuli), kama walikuwa na uhakika na jambo hilo kwanini walipeleka timu uwanjani! si wangebaki Dar tu na kuonekana wamejitoa, lakini walienda Iringa kwa shangwe kibao wakiwa na uhakika wa kushinda, na huyo msemaji wao kivuli akajitapa kuwa Azam wajipange mapema, kwani kule Lindi washabiki wote ni wetu, yaani wa kwao Yanga. Wakimaanisha tayari wana uhakika wa kuchukua kombe la FA. SASA IMEKUWAJE TENA!

    Bado Zahera wao akajisifu kuwa ........ Hao Lipuli walitufunga Yanga kwenye mchezo wa ligi wakati mimi sipo (Yaani Zahera yeye hakuwepo). Hiyo sababu inamaanisha kuwa bila yeye Yanga itaendelea kufungwa tu. Sasa sijui akiwepo yeye kuna kitu gani anakiongeza! au sijui ana nini cha kuleta ushindi!.

    Sasa leo alikuwepo na bado wamepigwa. Tena kwa kuwadhihirishia kuwa kwenye ligi hawakubahatisha, wamewapa Square ya ule ushindi wa awali mbele yake Zahera. SIJUI ATASEMAJE SASA. Mara oooh siku ile walibahatisha tu, hakuna hata shuti moja ambalo lililenga lango zaidi ya lile goli. Lopoka sasa!!!

    ReplyDelete
  11. Uongozi utathmini maendeleo na kwanini timu haijafanikiwa....ingawa ni kweli kuwa huyo kocha amewasaidia lakini lazima kuwepo na kubadilishwa na kuliimarisha benchi zima la ufundi...msiridhike kwakuwa mnaongoza ligi na mmefikia nusu fainali ya FA. Ukweli ni kwamba timu ina mapungufu mengi sana....caliber ya wachezaji wa Yanga wengine hawakufaa kuwemo kwenye hii timu wengi wao viwango ni vya chini mno, na umri umesogea mno. Pia mwalimu wa viungo, kocha wa makipa, madaktari, mameneja na wachua misuli....bado ni wa level ya chini hawana tofauti na wa timu za Ndanda, Alliance nk....usajili na viwango vya professional players ni duni....ndio unaweza ukadai kuwa tatizo ni pesa lakini hata hivyo baadhi yao hata scouting was very poor, na hawakuwa fiti, kuporomoka kwa uchezaji wao na umri umesogea mno, wachezaji wengi wazawa pia kuna kushuka kwa viwango kama ilivyo kwa wageni......timu kama Lipuli siyo ya kuitoa Yanga....yaliyopita si ndwele sasa tugange yajayo....USAJILI WA KIWANGO CHA JUU NA KULIIMARISHA BENCHI LA UFUNDI....Challenge ni kushawishi wachezaji waliopo ambao wameibeba timu kubaki kikosini....kwa kusaini mikataba mipya!....Kuhusu Uwezo wa Mwalimu Noeli Mwandila....sidhani kama unaridhisha....kila ambapo Mwalimu Zahera akiondoka kwenda kwenye timu ya Taifa Kongo....akirudi viwango vya wachezaji vinakuwa chini mno....physical fitness is very low!...lazima ili liangaliwe....madaktari pia wachezaji walio majeruhi Yanga huchukua muda mrefu kupona....nadhani kuna haja ya kuipa uwezo na vifaa vya kisasa idara ya utabibu....yako madhaifu mengi mfano mengine kama kutokuwepo kwa ubora wa kambi na viwanja vya mazoezi, na kadhalika lakini haya ndio ya msingi....sasa mengine yalichangiwa na uongozi dhaifu na uchumi kudorora sasa hivi au msimu ujao hilo lisiwe tena kisingizio!

    ReplyDelete
  12. Yanga walikuwa wanawacheka wanaume walivyotolewa kwenye shughuli ya kiume....sasa wao leo show ya kichana imewachania sketi...Jana Mlisema Prison kachukua mzigo vipi nyinyi leo mmechukua mzigo kwa Lipuli?? Msiwe mnawalaumu wenzenu kwa shughuli iliwashinda nyinyi..!

    ReplyDelete
  13. Mimi ni Yanga damu, ila muda mwingine lazima tuwe wakweli ili tusaidie timu. Timu ya Yanga ni Mbovu. Hii timu ilikuwa ikishinda kwa bahati bahati tu, watu wengi hawakufahamu kwa sababu ya ushabibi usio na mpango. Muro alishawahi kusema Yanga wachezaji wazee na Zaera sio Coach, Watu wakapiga sana kelele... haya sasa mambo yanajidhihirisha. Asilimia 80% ya wachezaji Yanga umri umewatupa mkono. ushauri ni kwamba, Benchi zima la ufundi la Yanga livunjwe na atafutwe Coach mwingine, Zaera awe FUND RAISER wa Yanga na sio Coach. sivyo tutakaa miaka mingi sana bila kushiriki michuano ya CUF.

    ReplyDelete
  14. hii post imepata comments nyingi sana

    ReplyDelete
  15. duh jamani Zuhura weee!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic