Kocha Mkuu
wa Yanga, Ernies Brandts amesema kikosi chake kilicheza vizuri na anawapongeza
wachezaji kwa uwezo mkubwa waliouonyesha.
Lakini amekiri
kwamba Chuji ndiye alistahili kuwa mchezaji bora wa mchezo kama walivyotangaza
Supersport.
“Timu
yangu inafanya kila kitu kama timu, tunashinda na kupoteza pamoja.
“Lakini
kitaalamu kuna mambo mengi sana, kuwa mchezaji bora we mechi ni kitu cha
kawaida na wala kisiwakatishe tamaa wengine.
“Chuji
alistahili kuwa mchezaji bora wa mchezo huo kwa kuwa alifanya kaiz kubwa.
“Kwanza
nasema bado kuna mambo ya kufanya Yanga, ninaamini msimu ujao tunaweza kufanya
vizuri zaidi,” alisema.
Salehjembe
ilikuwa ya kwanza kumtangaza Chuji kuwa mchezaji bora wa mechi ya watani, Yanga
na Simba, juzi kwenye Uwanja wa taifa, Dar.
Chuji
alicheza kama kiungo mkabaji na alichezesha timu huku akiongoza kwa kukaba na
kuwapa ahueni kubwa walinzi wa kati, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani.
0 COMMENTS:
Post a Comment