Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga wanatarajia kutua jijini Dar es Salaam
kimyakimya wakitokea Pemba walikoweka kambi ya siku kadhaa kujiandaa na mechi
dhidi ya watani wao Simba.
Yanga inashuka dimbani kucheza na Simba keshokutwa Jumamosi katika mechi
ya kufunga pazia la Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuwa kali nay a kuvutia.
Taarifa ambazo Salehjembe imezipata, Yanga itatua kesho asubuhi au mchana na kuweka kambi katika hoteli moja
maarufu jijini Dar.
Kinachowarudisha Yanga siku moja kabla ya mechi ni kuhakikisha wanafanya
mazoezi kwenye uwanja wenye nyasi halisi kama zle watakazozitumia kwenye Uwanja
wa Taifa Jumamosi.
Yanga imekuwa ikifanya mazoezi kwenye nyasi bandia mjini Pemba, hivyo
inaonekana kwao ni vema kufanya angalau kwa siku moja kwenye nyasi halisi.
Hata hivyo, uongozi wa Yanga umefanya safari hiyo siri kubwa na hautaki
ijulikane wanarudi lini.
Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto alisema hivi: “Bado tuko huku Pemba, suala
la kuja lini wanajua zaidi ni kamati ya utendaji.
“Lakini hapa Pemba ratiba ya mazoezi asubuhi.
“Kama ni nyasi bandia hata Azam wamekuwa wakifanya katika nyasi bandia
na kucheza katika nyasi za kawaida.”
0 COMMENTS:
Post a Comment