May 31, 2013



 
Pamoja na kwamba uongozi wa Yanga unaonekana kupata ugumu wa kumsajili mshambuliaji wake, Hamis Kiiza, taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zimeeleza, anatakiwa.

Anayemtaka Kiiza aendelee kubaki ni Kocha Mkuu, Ernie Brandts ambaye amewaambia viongozi anataka mshambuliaji wa aina yake.

“Kweli Kiiza amekuwa anatusumbua sana, anataka tumpe dola elfu hamsini. Hakika ni nyingi sana.

“Lakini kocha anaonyesha anamtaka kwa ajili ya msimu mwingine, hivyo tunaendelea kupambana.


“Kocha anasema Kiiza ni muhimu katika safu ya ushambuliaji, bado ameshikilia msimamo wake na mara ya mwisho alisema anataka dola elfu arobaini na tano,” kilieleza chanzo.

Kiiza amekuwa mmoja wa washambuliaji tegemeo wa Yanga ingawa baada ya kwisha kwa mkataba wake amekuwa akisisitiza kutaka dau kubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic