May 31, 2013



Kiungo Tinashe Tsungi raia wa Zimbabwe amejitokeza kuwania nafasi ya kucheza katika kikosi cha Simba.

Tsungi ,21, amesema amewahi kucheza soka katika klabu ya Jomo Cosmos ya Afrika Kusini lakini katika kikosi chake cha timu za vijana.

Mzimbabwe huyo ni kati ya wachezaji wanaowania nafasi ya kucheza Simba msimu ujao.

Simba inaendelea na mazoezi katika Uwanja wa Kinesi, Shekilango jijini Dar es Salaam.

Pamoja na Tsungi, Simba inawajaribia wachezaji wengine kutoka Ivory Coast na DR Congo.

Simba inajiandaa na michuano ya Kagame itakayofanyika nchini Sudan kuanzia mwezi ujao pamoja na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.  

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic