May 30, 2013



M To The P akiwa na Mangwea

 Baada ya kuwa katika hali mbaya, hatimaye M To The P amezinduka na kuanza kuuliza kuhusiana na rafiki yake Mangwea
M To The P alipelekwa kwenye wodi ya wagonjwa wa kawaida leo mchana.

“Kweli anaendelea vizuri sana, sasa amepelekwa kwenye wodi ya wagonjwa wa kawaida,” alisema Ruta Bushoke, msanii wa muziki wa kizazi kipya anayeishi nchini humo.


Lakini baadaye Mtanzania mwingine anayeishi nchini humo alisema M To The P amezinduka.

“Jamaa anauliza Ngwea yuko wapi, sasa tunashindwa hata kumjibu. Lakini kuna wengine wamemuambia kwamba atakuja hivi karibuni. Ametoka kidogo,” alisema.

Mangwea na M To The P walikutwa na mkasa ambao ulipelekea Ngwea kuaga dunia nay eye kubaki akiwa katika hali mbaya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic