May 30, 2013



 
Marehemu Albert Mangweha alikuwa shabiki mkubwa wa Manchester United ya England maarufu kama Mashetani Wekundu.


Pamoja na kuwa shabiki mkubwa wa Man United, Mangwea mara ya mwisho aliishangilia timu ya Borrusia Dortmund ya Ujerumani akita ishinde Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mangwea alitaka Dortmund iinyoe Bayern Munich ya Ujerumani pia katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Wembley jijini London.

Mangwea akiwa na M To The P na rafiki zake wengine, walijumuika na rafiki zao wa Afrika Kusini kwenda kuangalia mechi hiyo katika kitongoji kimoja jijini Johannesburg.

Hata hivyo, Bayern walitoka wababe kwa mabao 2-1 na kuwaacha Ngwea na rafiki zake wakiwa hawana la kufanya.

Mangwea alifariki dunia Jumanne jijini Johannesburg baada ya kukutwa amekata roho chumbani huku M To The P akiwa katika hali mbaya.

Mwili wa Mangwea unatarajia kuwasili nchini keshokutwa Jumamosi jioni na shughuli za kuuaga zitakuwa Jumapili, hii ni kwa mujibu wa familia yake.

Lakini Watanzania walio Afrika Kusini walikuwa wanaendelea na kikao leo mchana kujua nani atakayeshindikiza mwili wa Mangwea kurejea nyumbani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic