Dakika chache baada ya kuukosa Ubingwa wa FA kwa
kuchapwa na Wigan, Kocha Mkuu Man City, Roberto Mancini amesema uzushi mtupu
umetawala kuhusiana na nafasi yake kutaka kuchukuliwa na Kocha wa Malaga, Manuel
Pellegrini.
Lakini Mancini ameushambulia uongozi wa Man City
kwamba haukuonyesha juhudi zozote kwamba suala hilo ni uzushi kwa kufungua
mdomo na kulizungumzia.
“Naweza kusema huo ni upuuzi,” alisema Mancini
alipozungumza na kituo cha runinga cha ITV cha Uingerreza baada ya mechi dhidi
ya Wigan.
“Bado siwezi kujua ni kweli au la, lakini katika
soka kila kitu kinaweza kutokea. Lakini klabu imekaa kimya, haikusema lolote
kuhusiana na hilo kuonyesha kuzuia kuendelea kwa tetesi hizo, si kitu kizuri.”
“Bado nna miaka minne katika mkataba wangu, kama
itakuwa kweli kuhusiana na Pellegrini ni kweli, basi mimi ntakuwa mpuuzi.”
Hivi karibuni ilielezwa
uongozi wa Man City kupitia mmoja wa viongozi alikutana na wakala wa Pellegrini na kujadili
naye suala la kutua kuifundisha timu hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment