May 12, 2013




Inaonekana wazi kwamba Wayne Rooney ataondoka Manchester hasa baada ya mashabiki kuongeza chumvi katika kidonda chake.
Rooney amezomewa dakika chache zilizopita wakati akipokea kombe kwenye Uwanja wa Old Trafford.


Kila mchezaji alishangiliwa wakati anainua kombe hilo, ilipofika zamu yake mashabiki waligawanyika baada ya baadhi kumzomea na wengine kumshangilia.

Amekuwa mchezaji pekee aliyezomewa kati ya wote waliokuwa uwanjani hapo, huenda hiyo itachangia aendelee kulazimisha kupata uhamisho na kuondoka katika klabu hiyo.

Tayari Rooney ameishaomba kuondoka na katika mechi ya leo dhidi ya Swansea hakuwepo hata katika benchi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic