May 21, 2013


Nikiwa na Cafu wa Brazil, jamaa nilimhoji hata bila ya kupangiwa na hakuwa na noma..

Maisha ni safari ya aina yake, najaribu kukumbuka siku kadhaa zilizopita, sasa zinaonekana ni miaka tena.

Mwaka 2010 ulikuwa ni spesho kwa soka la Afrika, Kombe la Dunia lilifanyika kwa mara ya kwanza barani humu.
 
Saleh Ally na Marcelo Lippi baada ya mahojiano, alikuwa amekasirika baada ya waandishi wa Italia nao kulazimisha afanye mahojiano nao bila ya kufuata utaratibu...
Nilijua nisingeweza kupata fedha kwa kuwa sina uwezo mkubwa, nilianza kudunduliza kwa kuhifadhi kila nilichipata.

Mwanzo nilifanikiwa kupata nafasi ya kwenda katika upangaji wa makundi na ratiba zilizofanyika jijini Cape Town, Afrika Kusini.
 
Nikiwa ukumbini wakati wa upangaji wa ratiba...
Huko naweza kusema nilijifunza mengi sana, kwanza ni namna wenzetu walivyopiga hatua na namna ambavyo nchi za Afrika zinavyoweza kufanya mambo makubwa. 
  
Afrika Kusini ilifanya vizuri zaidi ya Ulaya, lakini bahati kwangu kama mwandishi wa habari.
 
Baada ya kumaliza kushiriki katika upangaji wa ratiba za Kombe la Dunia mwaka 2010 jijini Cape Town.
Nilikuwa mwandishi pekee kutoka Tanzania ambaye nilipata nafasi ya kuingia katika ukumbi na kuripoti upangaji huo wa makundi na ratiba.
 
Abeid Pele akiwa hatua chache na nilipokuwa nimekaa katika chumba cha mikutano
Lakini nikiwa nimekaa karibu kabisa na Abeid Pele na David Beckham, baadaye nilijiandikisha katika kundi la waandishi watakawahoji makocha.

Katika kuchagua, nilimchagua kocha wa mabingwa kutoka Italia, Marcelo Lippi. Alinipa ushirikiano mkubwa na mahojiano yangu yalikuwa bomba sana.
Nikipiga danadana nje ya Cape Town Stadium kabla haujakamilika..


Lakini pia nilifanya mahojiano na Cafu, nahodha wa zamani wa Brazil ambaye hakuonyesha nyodo ingawa sikuwa nimepangiwa kumhoji. 
Hakika nilijifunza mengi, najua ni vigumu kupata bahati kama hizo, lakini nilijifunza kumbe hata bahati hutafutwa, haziji ukiwa umelala nyumbani.

Ninaamini kuna nafasi na bahati nyingi zinawasubiri waandishi wengine, lakini lazima wakubali kugharimika na kujifunza au kupambana kukipata wanachokitaka kama ndoto.

Wakisema wasubiri msaada watafeli, wakiwaza kungoja kubebwa watapotea kabisa. Kazi ya uandishi ni ngumu, lakini kama unaipenda hasa, basi makubwa yanawezekana.

Usikubali kukatishwa tamaa, wako wengi wanaoamini waandishi ni watu wa kubahatisha, ukijiweka hivyo, utakuwa hivyo lakini mimi siko hivyo kwa kuwa sikutaka kuwa hivyo.
NAKUMBUKA ZAMANI!

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic