May 11, 2013




Vijana wawili wa kikosi cha timu ya vijana wa Azam FC wamepaa nchini Ujerumani kwa ajili ya kushiriki michuano maalum ya vijana.

Walioondoka jana ni Dismas Achimpate ambaye ni beki wa kati na Mudahir Yahya ambaye ni kiungo.

Mudahir ni kati ya wachezaji walioitwa na Kocha Kim Poulsen katika kikosi cha Young Taifa Stars.


Michuano hiyo pamoja na mafunzo mbalimbali yatawajumuisha vijana hao watakaoungana na wengine wa kituo cha kukuza vipaji cha TSC cha jijini Mwanza.





Vijana hao wameondoka usiku huu kwenda katika jiji la Frankfurt kupitia Addis Ababa, Ethiopia.
 


Wakiwa nchini humo kwa zaidi ya wiki 10, wachezaji hao watajifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata nafasi ya kuangaliwa na mawakala mbalimbali wa kuuza wachezaji wanaotambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa.

Kwa upande wa mawakala, Tanzania inawakilishwa na wakala maarufu Damas Ndumbaro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic