Na
Mwandishi Wetu
SHABIKI
mmoja wa Simba, ameshindwa kujizuia na kuangua kilio mbele ya Kocha Mkuu wa
Yanga, Ernie Brandts.
Mfanyakazi
huyo aliangua kilio wakati Brandts alipoamua kwenda kupata mlo wake katika hoteli
moja maarufu eneo la Masaki jijini Dar es Salaam.
Baada ya
kumuona Brandts, shabiki huyo haraka alimkimbilia na kumueleza kwamba anasikia
uchungu sana kuhusiana na Yanga kuifunga Simba kwa mabao 2-0 siku moja
iliyopita.
Shabiki
huyo alimueleza Brandts kwamba yeye ni Simba damu, lakini amejitokeza
kumpongeza Mholanzi huyo kutokana na kazi nzuri aliyoifanya.
“Kweli
amenishangaza,” alisema Brandts baada ya shabiki huyo kuangusha chozi. “Lakini
ameonyesha kiasi gani ni shabiki wa dhati wa Simba na anayekubali kazi
waliyoifanya Yanga.
“Soka ndiyo
iko hivyo, chochote kinaweza kutokea. Lakini kama kutakuwa na watu wanakubali
kazi za wenzao kama yule shabiki, basi hata maana ya soka itaonekana.”
Brandts
aliondoka siku hiyo na kurejea kwao Uholanzi ambako atakuwa katika mapumziko
hadi mwanzoni mwa mwezi ujao atakaporejea na kuanza maandalizi ya michuano ya
kimataiga na msimu mpya.
0 COMMENTS:
Post a Comment