May 22, 2013



 
Mabingwa watetezi mara mbili mfululizo wa Kombe la Kagame wametupwa kundi laini la C katika michuano ya kombe hilo itakayofanyika nchini Sudan kuanzia Juni 18 hadi Julai 2.

Wapinzani wao wakubwa, Simba wamepangwa kundi C lenye timu ngumu na italazimika kufanya kazi ya ziada ili kusonga mbele.

Yanga iko kundi C na timu za vibonde Ports ya Djibouti, Express ya Uganda na  Vital 'O'  kutoka Burundi. Lakini Simba wana kibarua cha kuzing'oa timu ngumu za wenyeji El-Mereikh, APR ya Rwanda na wabishi Elman ya Somalia.

Kundi B lina timu za Falcons ya Zanzibar, wababe wa Kenya, Tusker vibonde Al Nasir ya Sudan Kusini na wenyeji Al-Hilal.

Kawaida zawadi za Cecafa hugharimu dola 60,000 ambazo hutolewa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame.

Safari hii mambo yatakuwa mazuri zaidi kwa kuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji aliongeza dola 20,000 wakati Yanga ikiwa mjini Kigali na kupata nafasi ya kutembelea Ikulu ya Kagame, huku Salehjembe ikiwa ni blogu pekee iliyohudhuria katika hafla hiyo.

MAKUNDI:
Kundi A:
El-Mereikh
Simba
APR
Elman

Kundi B:
 Al-Hilal
Tusker
Falcons
Al Nasir

Kundi C:
Yanga
Express
Vital'O
Ports

RATIBA:
Juni 19, 2013
VitalO v Ports (Elfashar)
June 20: Yanga v Express (Elfashar)
Elman v APR (Elfashar)
Super Falcon v Al Nasir (Kadugul)
Tusker v Al-Ahly (Kadugul).
June 21, 2013
El-Mereikh v Simba (Elfashar)
Express v Vital '0' (Elfashar)
 
Juni 22, 2013:
Express v Vital 'O' (Elfashar)
Ports v Yanga (Elfashar)
Al Nasir v Tusker (Kadugul)
Al-Ahly v Al-Hilal (Kadugul)
Juni 23, 2013:
APR v Simba (Elfashar)
El-Mereikh v Elman (Elfashar)
Juni 24, 2013:
Al-Ahly v Al-Nasri (Kadugul)
Super Falcon v Al-Hilal (Kadugul)
Ports v Express (Elfashar).
Juni 25, 2013:
Vital '0' v Yanga (Elfashar)
Juni 26, 2013:
Al-Ahly v Super Falcon (Kadugul)
Al-Hilal v Tusker (Kadugul)
Simba v Elman (Elfashar)
El-Mereikh v APR (Elfashar).
Juni 27, 2013: Mapumziko
Juni 28, 2013: Robo Fainali
Juni 29, 2013: Mapumziko
Juni 30, 2013: Nusu Fainali
Julai 1, 2013: Mapumziko
Julai 2, 2013: Fainali na Mshindi wa Tatu



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic