Klabu ya AS Kaloum ya nchini Guinea imezidi kusisitiza kwamba El Hadji Diouf ni mchezaji wake.
Uongozi wa AS Kaloum umesema ulikubaliana na Diouf na amesaini mkataba wa kuichezea kwa miezi minne tu.
AS Kaloum imeamua kuweka msisitizo huo baada ya uongozi wa Leeds ya England kufafanua suala la mchezaji huyo na kusema bado ina mkataba naye wa mwaka mmoja.
Rais wa AS Kaloum, Boubah Sampil ametangaza kwa mara ya pili kwamba wana mkataba wa miezi minne na Diouf raia wa Senegal.
Tayari kumekuwa na mzozo mkubwa kuhusiana na suala hilo na ukweli bado ni tatizo.
Tatizo la kupatikana ukweli linatokana na Diouf kuamua kukaa kimya hasa kwa kuwa alimaliza vibaya msimu akiwa na Leeds baada ya kutolewa nje kutokana na kuonyesha ishara za kihuni kwa mashabiki wa Brighton.
Bado ukweli haujajulikana, lakini Leeds imekuwa na msimamo kuhusiana na mkataba huo wakati AS Kaloum ambao ni vinara wa soka la nchini hiyo kutoka jiji la Conakry wamesisitiza ni mchezaji wao.
0 COMMENTS:
Post a Comment