May 10, 2013




Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Wazee wa Yanga, aapenda
Kuwafahamisha kuwa Wazee wa Yanga wamefurahi na kuwashukuru Viongozi wa Klabu ya Yanga chini ya Mwenyekiti Yusuf Manji na Makamu
Mwenyekiti Clement Sanga kwa kuongoza Klabu na kuweza kunyakua Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu wa 2012/2013.

Ushindi huu umetokana na uongozi bora, uwajibikaji katika kutekeleza majukumu ya klabu na kufikia malengo.

Mwenyekiti wetu ametujengea dhana ya kuwa na imani ndani ya uongozi, wanachama na wachezaji wetu.

Hivyo basi na sisi kama wazee wa Klabu tunayo imani na viongozi na
wachezaji wetu na tunaahidi kuwa mchezo wetu wa tarehe 18 Mei 2013 kati yetu na Simba lazima tushinde ili tusherehekee Ubingwa wetu kwa furaha, shangwe na nderemo.

“YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO”

K.n.y: YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB na MWENYEKITI WA WAZEE
YANGA ALHAJ JABIRI M. KATUNDU

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic