Umewahi kuwa karibu na Patrick Liewig wakati kikosi cha Simba kinacheza? Unaweza ukajiuliza “huyu babu vipi!”
Mzuka wake ni noma, wakati mwingine anazungumza mwenyewe. Kwa kifupi yeye ni mtu anayetaka ushindi zaidi kuliko kitu kingine.
Hivyo anakuwa hatulii, mara akae hapa mara pale na mara nyingi hataki hata kidogo kukaa kwenye kiti chake kwenye benchi. Badala yake amekikabidhi kwa msaidizi wake Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
Lakini wakati Simba inacheza na Mgambo Shooting, Mfaransa huyo aliamua kukaa kwenye dumu maalum linalotumika kuhifadhi maji na vitu vya baridi.
Liewig alikaa juu ya dumu hilo na kusababisha baadhi ya mashabiki wa Yanga kuanza kuzomea wakimtuhumu eti ni muuza ice cream!
Hata hivyo, Simba ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na kuzidi kuipa hofu Yanga katika mechi yao ya Mei 18.
hahahahahahahahahahahahahahahah
ReplyDelete