June 26, 2013





Ujenzi wa hoteli ya kisasa na  ya aina yake umanza ndani ya bonde kubwa, inakadiriwa kuwa mita 100 kwenda chini. Imepewa jina la InterContinental Shimao Hotel.


Hoteli hiyo ya nyota tano inajengwa kwenda bonde linalomwaga maji lililo katika milima ya Tianmenshan nchini China na itakuwa na michezo mbalimbali itakayowavutia watu mbalimbali wakiwemo wanamichezo.



Hoteli hiyo itakuwa katika jimbo la Songjiang nchini humo na inatarajiwa kugharimu pauni milioni 345 hadi itakapokamilika.


Bonde lilivyo kabla ya kuanza ujenzi..

Mchoro wake umebuniwa na kampuni ya Atkins ambayo asili yake ni nchini Uingereza na ndani yake kutakuwa na vyumba 380, baadhi yake vikiwa chini ya maji.



Wakati sehemu ya maegesho ya magari huwa chini ya hoteli na vyumba vinakuwa juu, katika InterContinental Shimao Hoteli, maegesho yatakuwa kwenye paa la hoteli hiyo.

Sehemu ya paa hilo litakuwa ni majani na michezo kama kuruka katika maji na milima itapewa sehemu kubwa, pia mchezo wa gofu.

InterContinental Shimao inatarajiwa kuwa imekamilika ifikapo mwaka 2015 na inaelezwa bei inakadiriwa kuanzia pauni 200 sawa na Sh 520,000 kwa usiku mmoja.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic