June 26, 2013



Nsa akiwa kitandani siku chache baada ya kuumia vibaya wakati akiichezea Coastal Union...


Mshambuliaji nyota wa Coasta Union, Nsa Job amerejea uwanjani na kuanza kufanya mazoezi.

Nsa ana zaidi ya wiki mbili sas akifanya mazoezi mepesi yanayojumuisha kukimbia na kucheza mpira.




Akizungumza leo, Nsa amesema kuwa amekuwa akijisikia vizuri na anaamini ataweza kurejea katika kiwango chake kwa kuwa amekuwa akifuata maelekezo ya daktari wake.

“Kweli nimeanza mazoezi na sasa muda kidogo, nilikuwa nikifanya taratibu lakini sasa nacheza mpira angalau kidogo.

“Awali nilikuwa na hofu kubwa, lakini sasa nimepata matumaini kuwa huenda mambo yakaenda vizuri hapo baadaye,” alisema Nsa.
Nsa aliumia mwishoni wa raundi ya kwanza ya msimu uliopita na kulazimika kupelekwa nchini India.

Klabu ya Coastal Union ilimpeleka mshambuliaji huyo kutibiwa na sasa amefanikiwa kuanza mazoezi.

Mwenyewe ameeleza kwamba anajisikia yuko katika hali nzuri na anaamini atarejea katika kiwango chake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic