June 24, 2013



Kiungo nyota wa Tottenham, Gareth Bale ameonyesha wazi kwamba anataka kwenda Hispania na kujiunga na Real Madrid.

Pamoja na kocha wake, Andre Villa Boas kusema hatakwenda popote, tayari Bale ameuambia uongozi wa Spurs kwamba anataka kwenda Madrid.

Hali hiyo inasababisha kuongeza msukumo wa Spurs kufanya mazungumzo na Madrid ili kujua mustakabari wake.

Taarifa zinaeleza kwamba mabosi wakuu wa klabu hizo Daniel Levy na Florentino PĂ©rez  watakutana ndani ya siku chache na kulimaliza suala hilo.


Kiungo wa zamani wa Madrid, Zinedine Zidane ambaye pia anahusika na masuala ya usajili wa timu hiyo amekuwa akitilia mkazo suala la kumnasa Bale ambaye ni mchezaji bora wa Ligi Kuu England msimu uliopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic