June 25, 2013




Fernando Torres amesema mambo yamebadilika kwa kuwa anajiona anaanza kurejea katika hali ya kawaida.

Torres amesema kuwa ingawa inaonekana amefunga mabao manne katika mechi dhidi ya Tahiti ambayo si ngumu sana, lakini yeye anaamini ameanza kurejea vizuri.

“Najisikia mwepesi, nina uwezo wa kufunga mabao mengi sasa. Mwili wangu uko vizuri na nitaendelea kufanya vizuri.

“Angalia msimu wake wa kwanza na Chelsea, ulikuwa ni wakati mgumu kupindukia. Lakini nilijitahidi kuendelea kupambana na sasa mambo yamebadilika,” alisema Torres.

Torres sasa yuko Brazil na kikosi cha timu yake ya taifa ya Hispania akiendelea kupambana ili kufanikisha kubeba Kombe la Mabara na nusu fainali zitaanza Jumatano.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic