June 2, 2013

 Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Radhia Msuya akisaini kitabu cha waombolezaji.
 ...akisalimiana na Adam Juma.
...akizungumza na mama pamoja na baba mdogo wa marehemu Mangwea.
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Radhia Msuya amefika nyumbani kwa mama mdogo wa marehemu Mangwea Mbezi, Goige jijini Dar es Salaam, leo na kutoa neno.

Akizungumzia msiba wa Albert Mangwea alisema amesikitishwa sana na kama Mtanzania, amewapa pole ndugu, jamaa, marafiki na wanamuziki wote nchini.

Akizungumza katika msiba huo alisema: “Mtu anayefia hospitali na nyumbani ni tofauti, alitakiwa kufanyiwa uchunguzi, ubalozi unafanyia kazi kibali ambacho kinatarajiwa kupatikana kesho (Jumatatu), ili ikiwezekana mwili wa marehemu uwasili hapa nchini Jumanne.

“Taratibu zinazopitiwa ni za kawaida ila kwa kutokana na umaarufu wa aliyefariki ndiyo inaonekana hivyo, hata kama ingetokea hapa kwa mtu wa nchi nyingine utaratibu ungekuwa ni uleule.

“Nitoe wito kwa vijana kuwa wanapokuja Afrika Kusini wanatakiwa kufuata taratibu na kutoa taarifa ubalozini, hiyo inarahisisha kutoa msaada pindi kunapotokea tatizo,” alisema balozi Radhia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic