June 2, 2013

 
TIMU ya Bayern Munich imekamilisha kilichotegemewa na wengi kwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Ujerumani linalojulikana kwa jina la DFB-Pokal kutokana na kifunga Stuttgart mabao 3-2, juzi, hivyo kukamilisha jumla ya mataji matatu makubwa msimu huu.

Bayern imekamilisha mataji matatu kutokana na awali kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi Kuu ya Ujerumani ‘Bundesliga’.

Mabao ya mabingwa hao yalifungwa na Thomas Muller aliyefunga mawili na Mario Gomez, mechi hiyo ilihitimisha safari ya mwisho ya kocha wa timu hiyo, Jupp Heynckes ambaye anaiacha timu hiyo na nafasi yake inachukuliwa na Pep Guardiola.

Stuttgart ilionyesha upinzani na kufanikiwa kufunga mabao hayo kupitia kwa Martin Harnik.

Timu za Ulaya ambazo zimewahi kutwaa mataji matatu kwa mpigo ndani ya msimu mmoja ni Celtic mwaka (1967), Ajax  (1972), PSV (1988), Manchester United (1999), Barcelona (2009), Inter Milan (2010) na Bayern Munich (2013).

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic