June 2, 2013

 
LICHA ya kuwepo na taarifa kuwa Liverpool haina mpango wa kumuuza mshambuliaji wake, Luis Suarez, taarifa nyingine mpya ni kuwa klabu hiyo ipo tayari kumuuza lakini si chini ya pauni milioni 50 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 80.

Taarifa hizo zimekuja ikiwa ni muda ambao habari za Real Madrid kumuwania Suarez zinazidi kushika kasi, huku mchezaji mwenyewe akionyesha nia ya kuihama Liverpool.

Kiongozi mmoja wa juu wa Liverpool, amesema kuwa wanataka kumuuza Suarez kwa dau hilo kama walivyofanya kwa Fernando Torres aliyetua Chelsea mwaka 2011.
Jumanne iliyopita, Suarez alinukuliwa akisema kuwa kama ikija ofa nzuri kutoka Real Madrid hawezi kuikataa.
Siku kadhaa zilizopita Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers alikiri kuwa Suarez anaweza kuuzwa lakini inatakiwa dau liwe kubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic