Hispania imefanikiwa kuingia nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mabara baada ya kuichapa Tahiti kwa mabao 10-0.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Maraccana jijini Rio De Janeiro, Fernando Torres alitupia mabao manne.
Mabao mengine ya Hispania yalifungwa na David Villa matatu na David Silva (mawili), Juan Mata na mabingwa hao watetezi wa Kombe la Dunia wakautawala mchezo kupita kiasi.
Hata kabla ya mechi hiyo iliyobandikwa jina la David na Golliath, ilionekana Hispania ingeshinda kutokana na ubora wa kikosi chake.
Ndiyo maana Kocha Del Bosque akaamua kuwapumzisha baadhi ya wachezaji wake akiwemo kipa Iker Casillas na nafasi yake ikachukuliwa na Pepe Reina.
Mashabiki walikuwa wakiwashangilia Tahiti muda wote wa mchezo kuonyesha wakitaka angalau wapate hata bao moja.
Lakini ilikuwa vigumu kwao hata kufika katika lakini ilikuwa vigumu kwao hata kufika katika lango la Hispania.
0 COMMENTS:
Post a Comment