Mshambuliajki mwenye kasi wa
Wigan, Arouna Kone ametangaza kuwa yuko tayari kuihama klabu yake hiyo na kutua
Everton au Liverpool.
Kone raia wa Ivory Coast alikuwa
kati ya wachezaji waliokuja nchini na timu yake ya taifa kuivaa Taifa Stars
ingawa hakucheza pamoja na kupasha misuri mara kadhaa kama anaingia.
Kone ameamua kuondoka Wigan
ambayo imeteremka daraja hadi la wkanza ingawa aliisaidia kutwaa ubingwa wa
Kombe la FA.
Inaonekana Kone ana nafasi kubwa
ya kutua Everton kwa kuwa kocha wake wa zamani Wigan, Roberto Martinez amejiunga
na Everton kuchukua nafasi yaDavid Moyes aliyekwenda Manchester United.
Msimu uliopita, Kone alifunga
mabao 13 ikiwa ni msimu wake mzuri na Wigan baada ya kutua Wigan alitokea
Levante ya Hispania kwa kitita cha pauni milioni 3.5.
0 COMMENTS:
Post a Comment