August 21, 2020

 







Na Saleh Ally

KILA mtu anaweza kuwa na kila anachokiamini tofauti na mwingine na hii ndiyo raha ya kupishana mawazo kwa kuwa kila mmoja anakuwa anaamini kile anachokiwaza na kukiamini.

 


Mimi naamini tofauti kabisa na wewe kwamba, fedha ambazo Yanga wanazitumia kwa ajili ya usajili zingeweza kutumika kuwapatia angalau uwanja wa mazoezi, basi lingekuwa jambo zuri sana.


Yanga wamefanya usajili wa zaidi ya Sh milioni 500, najua, itakuwa ni siri kwa kila kitu lakini uhalisia na wachezaji wanaowasajili, hakuna ubishi kwamba fedha zimetoka nyingi sana na kama kungekuwa na mpangilio mzuri yangefanyika yafuatayo na faida ingekuwa kubwa sana.



Nafuu:

Yanga imesajili wachezaji wa bei kubwa sana, mmoja hadi kafikia Sh milioni 220 na ni mchezaji mzalendo. Bado kulikuwa na nafasi kubwa ya Yanga kupata mchezaji wa aina hiyo kwa bei nafuu zaidi.


Unaona, beki kama Bakari Mwamnyeto akisajiliwa kwa zaidi ya Sh milioni 200, lakini Yanga inaweza kupata mchezaji kama huyo, mfano beki Ame, kasajiliwa kwa Sh milioni 35 na unaona tofauti ya kiwango na Mwamnyeto si kubwa sana.


Maana yangu ni hivi, wachezaji wanaosajiliwa wangeweza kuwa na ubora unaofanana na wale ambao wamesajiliwa kwa fedha kubwa ambayo ingebanwa kidogo na kiasi chake kupelekwa katika maandalizi ya uwanja.


Naendelea kusema ninaweza kuwa tofauti na wewe, najua ungetamani kuona ushindi wa uwanjani kwa kuwa haujui maumivu ya timu kujiandaa bila ya kuwa na uwanja wake wa mazoezi.


Yanga ina timu za vijana na wanawake, hizi zote haziwezi kuwa na maandalizi mazuri kama hakuna viwanja vya mazoezi. Hivyo naendelea kusisitiza hili jambo ni si sawa.



Mashabiki wanapenda ushindi lakini bado viongozi wanaweza kuwa na hesabu za kufikia mbali kwa kuwa kuwa na mchezaji mmoja wa zaidi ya Sh milioni 200, halafu usiwe na uwanja wa mazoezi pia ni matatizo.



Wataalamu wa usajili:

Lazima kuwa na timu sahihi ya usajili, lazima kuwa na watu wanaojua usajili utafanyika kwa ajili ya leo, kesho na baadaye. Maana usajili kama utakuwa kwa ajili ya kuwafurahisha wanachama tu leo, basi hilo ni tatizo kubwa sana.


Kinachofanyika Yanga ni kushindana zaidi na Simba, hili ni jambo zuri kwa kuwa linaleta maendeleo. Na wadhamini wa Yanga, GSM hakika wanajitahidi sana na wanastahili pongezi lakini kutubaliane kwa kuwa hakukuwa na skauti ya muda mrefu kupitia wataalamu, basi unaona mambo yatakuwa mazuri sasa lakini baada ya miaka miwili ijayo, Yanga itaendelea kubaki ilipo.


Nasema itabaki ilipo kwa kuwa mchezaji huenda akaondoka, huenda asielewane na uongozi au huenda mkataba wake utaisha atakwenda kwingine lakini Yanga itabaki ileile isiyokuwa na uwanja wake wa mazoezi.


Yanga haiwezi kuwa kubwa bila hata uwanja wa mazoezi, inaweza kuwa kongwe na maarufu kwa kuwa haikidhi vigezo vya kuwa kubwa.


Lazima kujifunza, kwa viongozi wanaojua wanafanya nini, maendeleo hayawezi kuwa ya leo pekee. Lazima kujipanga kwa ajili ya leo lakini muelekeo wa kesho uwe na uhakika.


Wakati mwingine unaangalia, Yanga haishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na huenda nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa ni kuendelea kujenga timu, hili ni jambo sahihi. Lakini kama Yanga inataka kufanya bora zaidi kwa muda mrefu zaidi, uwanja ambayo ni sheria namba moja katika mchezo wa soka kati ya zile 17 ni muhimu sana.



Ukianza kutaja sheria 17 za mchezo wa soka, unaanza na uwanja. Hii inaonyesha kiasi gani uwanja unakuwa muhimu katika hili jambo.



Yanga tayari wana eneo kubwa sana ambalo walipewa zawadi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Maana yake kwa sasa hawahitaji kununua kiwanja kwa ajili ya kutengeneza uwanja wa mazoezi, badala yake ni suala la kuanza kuotesha nyasi, kutengeneza magoli lakini angalau sehemu ndogo ya kubadilishia nguo na baada ya hapo zinaweza kuanza hesabu za uwanja wa nyasi bandia. Sasa hapa inashindikana vipi?



Hesabu zingekuwa nzuri kwenye timu ya skauti, maana yake Yanga bado ingeweza kusajili wachezaji wazuri, wa kiwango kama hiki walichosajili na baada ya hapo ikapata angalau uwanja wa mazoezi ambao ungeweza kuanza kutumika wakati wa maandalizi ya mzunguko wa pili. Mtafakari.


 


 



30 COMMENTS:

  1. N mawazo ake .mm sikubalian kwa mengi Timu ngap Zina viwanja vizr lkn havina wachezaj wazur na wanaishia matopen??

    ReplyDelete
  2. Ebu andika hata habari za ihefu au kmc..kila kukicha yanga...tungejenga uwanja ungesema bora tutununue wachezaji..tunanunua wachezaji kujaribu kuboresha timu ili tupate wadhamini wengi kama timu ikifanya vizuri..ebu andika habari za simba day yako kesho...acha tusajiri

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bora umemwambia ukweli..anatumika sana na mikia huyu jamaa, kila jambo baya hulipeleka kwa yanga sijui kwanini aisee. Awe msemaji wa simba basi tujue moja

      Delete
  3. Hana mantiki. Ni mawazo yake lakini. Huwezi kujenga Brand ya timu kwa kujenga Uwanja. Kumbuka Brand ndio inayoleta fedha. Huoni Mikia wanajenga Brand kwa kununua mechi na wanafanikiwa?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na goli linakuwaje kona kama hamnunui! Mnajifanya wasafii kumbe kazi yenu kubweka tu

      Delete
  4. Yaani huyu manake kabla ya kuwa na wachezaji Yanga ingetaliwa ijenge Uwanja ndugu unajua Kama AcMilan na Inter Milan zinatumia Uwanja wa Manispaa,lkn ma superstar wengi ulimwenguni wamepita pale .Hapa shida so Uwanja Ni kwanini Wachezaji wazuri wapo wamekuja Yanga ?umeona Molinga wako kasuswa anataka tukae na michezaji mibovu Simba yako iendelee kutamba,kwa kukusaidia hata hao Simba hawajabadirika issue tu ya Morrison ni mfano bila kusahau Senzo usituhadae hizi makala zako why zinalenga Yanga Sana?

    ReplyDelete
  5. Huna jipya kwa Yanga; kibaraka unayefahamika

    ReplyDelete
  6. Unajua Kakangu hizi Team kwa Watanzania ni kama Dini ,ukiwa mkristo au Muislam kweli habari za upande wa pili siyo issue ,mkubwa mimi utanishangaa Waandishi/Watangazaji wengi mnapenda simba tena ni Wanachama Yanga mnaitaja just bsness tunaishi na ninyi .Hapa fanya bsness pls .Uwanja utajengwa tu kwanza kama hujui Yanga imekuwa na Uwanja siku nyingi Kaunda mpaka Wizarani unatambulika issue ni kuukarabati.

    ReplyDelete
  7. Hizo ndizo akili za Gongowazi za kuchupa hatua elfu kabla ya kukata hatuna moja. Hapo ilikuwa shabaha kubwa kuikomoa Simaba ambayo kwa busara kubwa, walimaliza ya muhimu Kwanza halafu ndio wakayafanya waliyofanya. Vipi utavaa koti Kwanza kabla ya kuvaa shati?

    ReplyDelete
  8. Hawa wanatumika Sana kutuvurugia Wachezaji Kama siyo kuwarubuni ,inakera sana

    ReplyDelete
  9. TIMU IKIWA VIZURI NA IKAFANYA VIZURI ITAKUWA RAHISI KUTENGENEZA FEDHA NYINGI NA KUPATA WAFADHILI WENGI KIASI KWAMBA KUJENGA UWANJA ITAKUWA NI KAZI NYEPESI. NANI ANAWEZA KUTOA FEDHA ZAKE AMA UFADHILI(SPONSORSHIP) KWENYE TIMU INAYOSUA SUA? YANGA IKIFANYA VIZURI UWANJANI WAFADHILI NA HATA WANACHAMA UNAWEZA KUWASHAWISHI WAICHANGIE TIMU

    ReplyDelete
  10. Mimi niliwashtukia siku nyingi,niwarudishe nyuma wakati Kocha Maximo anafundisha Taifa Stars alisema hamtaki Juma Kaseja kwa ubinafsi
    Akawa hampangi ikaenda zaidi hata mwisho hakuwa anamwita National Team wakawa wanamsakama kwamba ana Uyanga ,sasa alipoondoka akapewa Kocha mwingine ndugu zangu nakumbuka alipo ita National Team akamtaja Wahandishi walishangilia utafikiri siyo reporters mimi kwa upande wangu na Uelewa wangu kilikuwa kituko fulani

    ReplyDelete
  11. Salehe, usiumize kichwa Senzo ameondoka Simba na napata sana wasiwasi na ile interview yako na Morrison

    ReplyDelete
  12. Wewe unaye penda matusi tu Gongo wazi kila muda,Hiyo Simba hata share alotment mnashindwa nakupa siri huyu jamaa matumizi ana record nadhani mpaka sass hv ameisha tumia B20 bado b29 ninyi zenu bado mnakaa kukenua meno tu

    Unatuletea vitumbo heti mpo stage ipi ya kutamba nayo mtu yupo Kamati ya Usajili na kahusika kumsajili mchezaji halafu eti mjumbe wa Kamati na analazimisha kushiriki maamuzi , kwa hiyo mmepiga hatua gani ya kutuaminisha sisi Wajinga au ile sebule pale Bunju ? Acheni Uswahili buana.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyu mtu anakesha kuikosoa yanga kwa kila jambo ambalo linafanyika hata kama ni zuri,kwake ni mbaya.ikijenga kwanza utasikia:wanatengeneza kwanza wachezaji hakuna upuuzi tu.salee aache yanga nao wapumue

      Delete
  13. Ngoja nikukumbushe jambo kidogo binaadam kusema au kukosoa ndio kawaida yake hasa nyinyi mnaojiita waandishi wa habari kwanza hao Yanga wasingesajili vizuri pia ungewasema leo wamesajili unawasema sasa unataka wafanye nini hasa?

    ReplyDelete
  14. Lakini mwanyeto ni wa kusajiliwa kwa 200,000,000 kweli? Tuwe wakweli kuna wakati mihemko inatawala

    ReplyDelete
  15. Wakianza kuchambua Simba kwenye Fm Redio na Azam utadhani Simba Barcelona inavyo pambwa.Mimi nililoona Simba pamoja na uzuri wanategemea Sana msaada was marefa,halafu marefa nao wanawaogopa ukiwaumiza hupangwi kuchezesha .

    ReplyDelete
  16. Naunga mkono kabisa, mimi ningetamani kabisa timu yangu ya Yanga, ingepotezea hata miaka miwili ubingwa tukasajili wachezaji wenye vipaji tu kwa gharama ndogo tukajenga timu. Harafu hizo bilioni tunazoshindana na Simba tukajenga uwanja, tena hata kwa kutuchangisha wananchi kama kawaida yetu.

    ReplyDelete
  17. Kwani hizo 200m ,si Ni pamoja na ada ya uhamisho brother kwa taarifa yako baada ya Kasa Mussa kuwashika masikio Coastal wakataka transfer fee na siyo uswahiba na Uswahili Kama ninyi na AZAM ,Thiimba mkachemka,sasa kwa ukweli pale kwenu nani beki anayelingana na Bakari.au ni yule zinjanthropas

    ReplyDelete
  18. Beki tegemeo National Team,kwa taarifa asingesajili Yanga angekuwA best defender.Maana alivyokuwa ana pambwa kabla ya kujua Yanga atashinda mbio hizo Ni balaha

    ReplyDelete
  19. Media oneni aibu Simba inawaharibia taaluma

    ReplyDelete
  20. Maoni yako siyo lazima yawe ya kweli unaweza ukawa wrong vilevile

    ReplyDelete
  21. Ingelikuwa tumeanza na uwanja bado ungekosowa na kusema Kamba tutafute wachezaji kwanza. Kwaiyo bado wewe ni kigeugeu wa maneno kwenye kuikosoa yanga why?

    ReplyDelete
  22. SALEH ALLY WEWE HUNA LOLOTE UNACHOJUA USHABIKI WA SIMBA UNAKUSUMBUA, ULITAKA YANGA ISAJILI WACHEZAJI WA KAWAIDA ILI IFUNGWE KILA MARA NA SIMBA, TUMESAJILI TIMU IMARA INAYOWEZA KUMPA UPINZANI WA KUTOSHA SIMBA NA AZAM NA KUPITIA MAFANIKIO TUTAKAYOPATA WANANCHI TUTAPATA HAMASA YA KUICHANGIA TIMU YETU KWA KUNUNUA BIDHAA MBALIMBALI ZA GSM PAMOJA NA YANGA NA KUJAZA VIWANJA HATIMAE PESA ZITAKAZO PATIKANA ZITAJENGA UWANJA. SALEH ALLY ENDELEA KUJIDANGANYA ILA TULISHAKUJUA KITAMBO WEWE NI MMOJA WA MAADUI WAKUBWA WA YANGA, JIHADHARI SANA IPO SIKU UTAJUTA KWANINI ULIKUWA UNATUMIKA KUIVURUGA YANGA.

    ReplyDelete
  23. Tukutane tarehe 18,hapo timu kubwa itajulikana kwani huyo mlombeba kama watumwa hana hela ya kununua marefu, mwendo ni uleule mechi za mwanzo mnatengeneza muunganiko wa timu cc ambao timu na kocha ni walewale tunawatimulia vumbi

    ReplyDelete
  24. nyinyi tuwajua ni simba na mnakakati wewe salehe masudimaestulo saidi kazumali na shaffih dauda mpo kwa ajili ya kuidhofisha yanga kila kinachofanyika yanga kwenu ni kibaya acheni unafiki

    ReplyDelete
  25. Kwenye hili brother upo wrong , Uwanja wa Mazoezi hata ule wa Simba haukidhi viwango ,wewe ungewashauri Simba walipe /au wamalize alotment au mgawanyo was hiaa kabla ya kujenga Bunju cse ,humiliki haujakamilika kuliko sajili na malengo yasiyo ya Kisoka,ungetegemea uwekezaji wa PSG icheze UEFA final baada ya miaka kumi?au Man City pamoja na mkwanja walokuwa nao wanaendelea kuhaha kutafuta Kombe la UEFA.Mnaweka mtu anaongea eti our target Ni semi final.Angalizo mechi ya nkana hapa Dar refa yule wa Kenya mnajua mlimpa nini mkirudia tunatoa taarifa CAF .

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic