June 20, 2013



 
Messi akiwa na baba yake, Jorge

Mshambuliaji nyota wa Barcelona ya Hispania, Lionel Messi atapanda kizimbani Septemba 17 mwaka huu kujibu mashitaka ya kukwepa kodi nchini Hispania.

Mecci atapanda kuzimbani pamoja na baba yake mzazi Jorge Horacio Messi, wote wawili wakituhumiwa na kukwepa kodi inayokadiriwa kufikia euro milioni 4.


Taarifa zinaeleza, Messi na baba yake walikwepa kodi kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia 2007, 2008 na 2009, huku wakijua kufanya hivyo ni uvunjifu wa sheria.

Messi na baba yake wanaelezwa kukwepa kodi wakati walipolipwa mamilioni ya euro kwa ajili ya kuuza haki ya picha yake kutumiwa katika nchi mbalimbali nje ya Hispania.

Kawaida walitakiwa kulipa kodi kwa kila mikataba waliyoingia, lakini wao walijikausha na kuchukua fedha zote walizolipwa bila ya kulipa kodi.
Tayari Messi ameishalizungumzia suala hilo na kusema yeye na baba yake hawana hatia na kila kitu walifuata utaratibu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic