June 26, 2013



 Chelsea maarufu kama The Blues wamefanikiwa kumnasa mshambuliaji nyota wa Bayern Leverkusen, Andre Schurrle.

Schurrle mwenye miaka 22 na mchezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani amesaini mkataba wa miaka mitano.

Pia mshambuliaji huyo amekuwa ndiyo wa kwanza kusaini Chelsea ikiwa chini ya kocha mpya, Jose Mourinho raia wa Ureno.


Hata hivyo Schurrle atakuwa na kazi ya kupambana kuwania namba na washambuliaji lundo wa Chelsea kama Juan Mata, Eden Hazard, Oscar na Kevin De Bruyne.

Mshambuliaji huyo Mjerumani tayari amekabidhiwa jezi namba 14 na alipachika mabao saba katika mechi 24 za timu ya taifa ya Ujerumani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic