Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia,
Kundi C, Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Ivory Coast (The
Elephants) iliyochezwa jana (Juni 16 mwaka huu) imeingiza sh. 502,131,000
kutokana na watazamaji 57,203.
Tiketi za kushuhudia mechi hiyo
ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh.
30,000.
Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama
ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh.
76,596,254.24 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 7,809,104.
Asilimia 15 ya uwanja sh.
62,658,846.26, asilimia 20 ya gharama za mechi sh. 83,545,128.35 na asilimia 5
ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 20,886,282.09.
Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 250,635,385.06 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,531,769.25 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo
wa TFF.
Mechi iliyopita ya Stars dhidi ya
Morocco (Lions of the Atlas) kwenye uwanja huo iliingiza sh. 226,546,000.







0 COMMENTS:
Post a Comment