June 23, 2013




Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga wataanza kujiandaa na msimu mpya jijini Dar es Salaam halafu baadaye watahamia Mwanza.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinaeleza, uongozi umepitisha timu hiyo kuweka kambi jijini humo ambako itapata mechi za kirafiki.

“Kweli haya ni mambo ya awali, tunaona Mwanza itakuwa sehemu nzuri kwa ajili ya kuweka kambi.


“Nafikiri hakutakuwa na mabadiliko na kocha aliishataarifiwa kuhusiana na suala hilo la kambi.

“Mechi za kirafiki ni muhimu pia lakini bado hatujajua tutacheza na timu gani,” kilieleza chanzo.

Awali Yanga ilianza maandalizi ya Kombe la Kagame, lakini ikajitoa kutokana na suala la usalama kwa kuwa mji wa Darfur nchini Sudan umewatia hofu kutokana na suala la usalama.



Kambi itaanza jijini Dar Julai 2 baada ya hapo Julai 7 Yanga itahamia Mwanza kuendelea na kambi ambako pia itacheza mechi za kirafiki.
 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic