June 23, 2013





Kiongozi wa Yanga, Mohammed Bhinda, jana alionyesha ‘fairplay’ ya nje ya uwanja baada ya kupanda jukwaa na kupokea tuzo ya kiungo wa Simba, Amri Kiemba.

Kiemba alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa Sputanza katika hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Baada ya kutangazwa, Kiemba hakuwepo ukumbini na ilionekana alikuwa akisubiriwa angalau kiongozi wa Simba kwenda kupokea.

Hata hivyo, hakukuwa na kiongozi wa Simba aliyekuwa ukumbini hapo na ilikuwa vigumu kwa viongozi wa TFF kuchukua tuzo hiyo kwa kuwa wao walikuwa wageni waalikwa.


Hivyo Bhinda alijitosa na kwenda jukwaani na kupokea tuzo hiyo ya Kiemba.

Baada ya hapo, baadhi ya watu waliokuwa ukumbini hapo walikuwa wakimtania kwamba amechukua tuzo ya watani wake.

Hata hivyo Bhinda alionekana kutokuwa na hofu na badala yake akarejea alipokuwa ameketi na tuzo hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic