Hatimaye Bayern
Munich imeshinda vita ya kupambana kumpata kumpata msshambuliaji Thiago
Alcantara.Mabingwa hao wa Ulaya wamemwaga kitita cha pauni milioni 22 kumnasa kinda huyo wa Barcelona aliyekuwa anawaniwa kwa udi na uvumba na mabingwa wa England, Manchester United.
Biashara hiyo ya Thiago imekamilika leo ikiwa ni pamoja na timu hizo kuingia mkataba wa kucheza mechi za kirafiki.
Kocha David Moyes wa Man United alikuwa anamuwania mshambuliaji huyo kwa juhudi kubwa lakini amekwama.
Inaonekana ushawishi wa kocha mpya wa Bayern, Pep Guardiola umechangia Thiago kujiunga na Bayern kwa kuwa alikuwa kocha wake walipokuwa Barca.







0 COMMENTS:
Post a Comment