July 25, 2013



 Hatimaye mshambuliaji Papiss Cisse wa Newcastle amekubali kuvaa jezi yenye wadhamini wa klabu hiyo.

Cisse raia wa Senegal alikosa mazoezi ya timu hiyo kwa zaidi ya wiki moja kutokana na kupinga kuvaa jezi yenye jina la Wonga ambao ni wadhamini wa klabu hiyo.


Wonga ni kampuni inayojihusisha na utoaji mikopo hivyo inategemea riba kwa ajili ya kujiendesha wakati imani ya dini ya Kiislamu ambayo Cisse ni muumini wake inakatakaza.

Lakini siku chache baada ya picha yake kunaswa akiwa casino na blogu hii pia ikairusha, Cisse hatimaye amekubali kukaa meza moja na uongozi na kufikia mwafaka wa suala hilo.

Anategemea kuanza mazoezi akiwa amevaa jezi yenye nembo ya Wonga na pia ataonekana baadaye katika mechi kadhaa za timu hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic