Hii ni kufuru, sasa Real Madrid imeamua kukata mzizi wa fitna na
sasa imeweka dau la pauni milioni 82 kumsajili kiungo nyota wa Tottenham, Gareth
Bale.
Lakini Spurs wameamua kufanya kikao cha dharura kujadili suala
hilo ambalo linaonekana kuwashtua.
Mshtuko wenyewe unatokana na dau kubwa waliloweka Real Madrid,
maana yake inaonekana itakuwa ni vigumu kulikataa.
Mchezaji pia anaonyesha anataka kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya
akiwa na wachezaji wengine nyota kama Ronaldo na Ozil.
Kama Spurs watakubali, maana yake uhamisho huo utakuwa ni rekodi
ya dunia.
Anayeshikilia rekodi hiyo ni Cristiano Ronaldo aliyejiunga na Real
Madrid kwa pauni milioni 80 akitokea Manchester United.
Baada ya Spurs kuzungusha kwa muda mrefu, hatimaye Madrid wameamua
kuvunja rekodi ya dunia ya uhamisho na kuweka dau hilo kubwa.
Katika hali halisi inaonekana Spurs hawana ubavu wa kupindua na
Bale mwenyewe ameonyesha wazi kwamba ni njia moja kwenda Madrid.
Wiki iliyopita, Bale hakuwa katika kikosi cha timu hiyo
kinachofanya ziara nchini Hong Kong na Kocha AVB akasema anasumbuliwa na misuri
kitu ambacho kinaonekana si sahihi.
Hali halisi ni kwamba Bale hayuko vizuri kisaikolojia kuhusiana na
suala lake hilo la uhamisho.
0 COMMENTS:
Post a Comment