Bosi mpya wa Bayern Munich, Pep
Guardiola alimchapa kibao kiungo mpya wa timu hiyo, Thiago Alcantara ambaye pia
ni raia wa Hispania kama kocha huyo.
Guardiola ndiye alimshawishi Alcantara
kujiunga na timu hiyo akitokea Barcelona aliyowahi kuifundisha pia kabla ya
kujiuzulu.
Guardiola alifanya hivyo wakati wa
mechi ya Kombe la Super Cup la Ujerumani dhidi ya wapinzani wakubwa Borussia
Dortmund, wakati akiwa anatoa maelekezo katika mechi hiyo ngumu ambayo BVB
wanaovaa jezi za njano na nyeusi walishinda.
Kocha huyo alionyesha ana hasira wakati
akizungumza na wachezaji wake ambao tayari walikuwa wamefungwa na alimuangalia
Alcantara na kumpa maelekezo kabla ya kumzabua.
Hata hivyo inaonyesha kibao hicho cha
Guardiola kililenga kumshitua kiungo huyo kutokana na kuonyesha kutochangamka
au kufuata alichokuwa amemueleza awali na si vinginevyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment