BAADA ya kuripotiwa kwa siku kadhaa
juu ya Klabu ya Bayern Munich kumuwania beki wa Chelsea, David Luiz imefahamika
kuwa Kocha wa Bayern, Pep Guardiola amejitoa kwenye mchakato wa kumuwania
mchezaji huyo.
Awali ilielezwa kuwa dau la Luiz raia
wa Brazil ni pauni milioni 40 lakini sasa Chelsea wameongeza na kutaka walipwe
pauni milioni 60 ili wamuachie mchezaji huyo, kitu ambacho Bayern wameona siyo
sahihi kwao.
Guardiola amekuwa akimuhitaji
mchezaji huyo kutokana na kuhisi safu yake ya ulinzi hasa beki wa kati
haijatulia, ndiyo maana akawa tayari kutoa pauni milioni 40 au ikiongezeka iwe
milioni 45 na si vinginevyo.
Luiz alitua Chelsea kwa pauni milioni
21.3 akitokea Benfica ya Ureno mnamo Januari mwaka 2011.
0 COMMENTS:
Post a Comment