MSHAMBULIAJI wa Yanga, Didier
Kavumbagu, raia wa Burundi, amekiri kuwa kutakuwa na ushindani mkubwa wa namba
katika nafasi ya ushambuliaji msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, lakini akasisitiza
kuwa amejipanga vizuri.
Kavumbagu
ambaye msimu uliopita alifunga mabao 10, yakiwa ni mengi zaidi ya mchezaji
yeyote wa Yanga, amesema msimu ujao
anaamini atakuwa na kasi zaidi ya ufungaji kuliko msimu uliopita.
Amesema
atajipanga vyema kwa kuhakikisha anafanya mazoezi kwa bidii ili aweze
kumshawishi kocha ampange.
“Ninakubali hali ya ushindani itakuwepo kwenye
safu ya ushambuliaji ukizingatia nyuma yangu kuna wachezaji Mrisho Ngassa, Said
Bahanuzi, Jerryson Tegete na Hussein Javu.
“Nitajituma
kwa nguvu zangu zote kuhakikisha sipotezi nafasi yangu,” alisema Kavumbagu.
0 COMMENTS:
Post a Comment