Kocha wa zamani wa Simba, Patrick Liewig amesema ana hofu kama viongozi wa Simba watamlipa fedha zake zilizobaki.
Lakini akawasisitiza kwamba ni vizuri wakaonyesha uungwana na kumlipa dola 10,000 anazodai pindi itakapofikia wakati wanataka kufaya hivyo.
Liewig raia wa Ufaransa amesema ameshitushwa sana na taarifa ambazo amekuwa akizipata kutokaka kwa watu wa karibu na uongozi wa Simba.
"Wananiambia uongozi una mpango wa kukaa kimya na fedha zilizobaki, naomba wanilipe kwa amani ili mambo na uhusiano wetu uendeelee.
"Watu wameniambia, yanaweza kuwa maneno lakini wengine ni wale wanaoheshima. Hivyo wasiache kunilipa ili kuonsha wanaithamini kazi niliyofanya," alisema Liewig ambaye yuko kwa Ufaransa.
Liewig alilipwa dola 10,000 ikiwa ni sehemu ya deni analodai kutokana na mshahara wake akiwa anainoa Simba kabla ya kutupiwa virago.
0 COMMENTS:
Post a Comment