KLABU ya Simba imepanga
kumpeleka kiungo wake mshambuliaji, Mwinyi Kazimoto, katika kikosi cha
Recreativo do Libolo cha Angola.
Simba imepanga kufanya hivyo, baada ya kubaini kuwa klabu hiyo inamhitaji kiungo huyo.
Kiungo
huyo hivi karibuni alitoroka kwenye kambi ya Taifa Stars na kutimkia Qatar
kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.
Akizungumza
na Championi Jumatano, Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili ya timu hiyo, Zakaria Hans Pope, alisema Libolo imeonyesha nia ya
kumsajili kiungo huyo, hivyo watampeleka huko kwa ajili ya majaribio.
Hans
Pope alisema kama timu hiyo ikiridhika na kiwango cha kiungo huyo, basi watakaa
meza moja kwa ajili ya kufanya mazungumzo katika dau la usajili.
“Libolo
imeonyesha nia ya kumsajili Mwinyi, hivyo tumepanga kumpeleka huko. Kabla ya
kusajiliwa, atafanya majaribio,” alisema Hans Pope.
0 COMMENTS:
Post a Comment