July 25, 2013




Kocha Mkuu wa Yanga mabingwa wa Tanzania Bara, Ernie Brandts amesema anataka kikosi chake kicheze mechi nyingine mbili za kimataifa.

Brandts amesema kama watapata mechi hizo mbili wakati kikosi chake kikiwa kimekamilika itamsaidia sana kujua ajipange vipi.

“Nafikiri litakuwa jambo zuri kwa kuwa tutacheza tukiwa kamili, ukiangalia mechi tulizocheza awali tulikuwa hatuna zaidi ya wachezaji sita ambao wako katika kikosi cha timu ya taifa.

“Lakini bado zimekuwa ni mechi zenye msaada na zimetupa nafasi ya kuona tumefanya vipi,” alisema.



Brandts ambaye ni Mholanzi alisema tayari ameishazungumza na uongozi wa Yanga ambao utalifanyia kazi suala hilo.

Yanga ilicheza mechi tatu za kirafiki za kimataifa, zote na timu kutoka Uganda, ikianza mbili dhidi ya Express, ikatoka sare jijini Mwanza na kupoteza mjini Shinyanga.

Halafu ikaridi jijini Dar es Salaam na kuivaa URA na kutoka nayo sare ya mabao 2-2 huku Yanga ikisawazisha mwishoni kupitia Jerry Tegete.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic