July 25, 2013





Kocha Kim Poulsen amesisitiza pamoja na kutokuwa na timu, nahodha wake, Juma Kaseja ataanza katika mechi ya Jumamosi dhidi ya Uganda.

Kim amesema Kaseja ndiye kipa wake namba moja, hivyo hatakuwa na namna zaidi ya kumpa nafasi hiyo.

“Kama tunazungumzia msimu huu maana yake unajumlisha na mechi inayokuja dhidi ya Uganda, Kaseja ndiye kipa namba moja,” alisema Kim kutoka Kampala.

Tayari Stars imetua mjini Kampala tayari kwa mechi hiyo ya Jumamosi kuwania kucheza fainali za Chan zitakazopigwa nchini Afrika Kusini.
Katika mechi ya kwanza, Stars ililala kwa bao 1-0 jijini Dar, hivyo inalazimika kushinda kuanzia mabao mawili huku ikifanya ulinzi imara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic